Seventh-day Adventist® Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

UTANGULIZI

Tunamshukuru sana Mungu wa kutulinda na kutuwezesha kumaliza miika miwili salama kabisa tangu ilipoanzishwa union yetu ya kaskazini mwa Tanzania, tunakiri kuuona mkono wa Mungu katika idara yetu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ifuatayo ni taarifa ya idara ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano ikieleza majukumu ya idara, mafanilio ya idara , changamoto za idara na mipango ya idara ya mawasiliano kwa uongozi mpya utakao anza kazi miaka mingine mitano ijayo

MAJUKUMU YA IDARA YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

  1. Kutoa habari na taarifa
  2. Mahusiano na Umma
  3. Kusimamia vyombo vya habari
  4. Udhibiti dhahama
  5. Kutumia mtandao kusambaza ujumbe wa malaika watatu 

MAFANIKIO YA IDARA TANGU JANUARY 2014 – JUNE 2015

  1. Kuanzisha tovuti ya unioni www.ntucadventist.org
  2. Kuanzisha mitandao ya kijamii ya facebook na twitter ambayo ni www.facebook.com/ntucadventist na www.twitter.com/ntucadventist
  3. Kuanzisha Studio na kituo cha kurekodi matangazo ya radio na nyimbo za injili kiitwacho NTUC Adventist Media Center
  4. Kuanzisha mafunzo ya komputa katika makanisa mbalimbali katika union ya kaskazini mwa Tanzania, jumla ya vituo 12 vimeanzisha na jumla ya wahitimu 134 wamehitimu mafunzo ya awali ya komputa
  5. Kuendelea kusajili website mpya za makanisa ya Waadventista Tanzania, jumla ya makanisa 176 yamesajiliwa na kuwa na tovuti za kanisa zinazotengenezwa kwa mfumo wa kanisa uitwao netAdventist. netAdventist ni mfumo wa kutengeneza tovuti za kanisa la Waadventista wa Sabato duniani bila kutumia gharama yeyote.
  6. Kutengeneza Gazeti la maranatha linalopatikana kwa njia ya mtandao
  7. Kurusha matangazo ya moja kwa moja ya siku ya vijana duniani kutokea Tanzania, tarehe 21/03/2015. Matangazo hayo yaliruka kwa ubora wa kiwango cha juu na kuonekana ulimwengu mzima kupita internet na Television ya Hope Channel
  8. Tarehe 7/7/2014 Television ya Morning star ilianza rasmi kurusha matangazo yake katika anga la Tanzania, huu ni mbaraka mkubwa sana ambao Mungu ametupatia
  9. Uanzishwaji wa Adventist Church Management System (ACMS) katika nchi ya Tanzania. ACMS ni mfumo wa usimamizi wa makanisa ya Waadventista wa Sabato duniani, Mfumo huu unatunza kumbukumbu za makanisa, washiriki, viongozi na wachungaji kuanzia ngazi ya kanisa mahalia hadi makao makuu ya kanisa duniani. Mfumo huu ndio rasmi wa kutunza kumbukumbu kwa kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwengu mzima. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambayo inatumia mfumo huu kutunza kumbukumbu zake. Mwaka 2015 kanisa la Riverside lililopo Arusha Tanzania lilitangazwa ndio kanisa linaloongoza barani Afrika kutunza kumbukumbu zake vizuri kupitia mtandao wa ACMS.
  10. Utengenezaji wa program tumishi za Nyimbo za Kristo na Ibada. Programu hizi zimerahizisha upatikanaji wa kitabu cha nyimbo katika simu pamoja na muongozo wa kujifunza biblia katika simu za Waadventista wengi hapa Tanzania.
  11. Mkutano wa kwanza wa TAiN Juni 22 – 24, 2015. TAiN ni kifupi cha maneno ya kingereza yaitwayo Tanzania Adventist internet Network ambayo humaanisha Mtandao wa Intaneti wa Waadventista Tanzania, Lengo la mkutano huu ni kujadili ubunifu na njia za teknolojia ya mtandao ili kutimiza utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato. Jumla ya watu 204 walihudhuria kutoka unioni mbili za Tanzania wakiwapo wachungaji, viongozi wa idara ya mawasiliano kanisani, makarani wa kanisa, IT, waandishi wa habari, wakurugenzi wa idara ya mawasiliano na makatibu wakuu wa konferensi, mkutano huu ulifanikiwa kwa kiwango cha juu na kuanzisha maazimio ambayo ni dira kwa viongozi wapya wa idara ya mawasiliano katika miaka ijayo.
  12. Kuanziasha radio ya mtandao ijulikanayo www.ustream.tv/channel/ntucmedia

CHANGAMOTO ZA IDARA

  1. Elimu ndogo ya teknolojia kwa washiriki wetu
  2. Ukosefu wa fedha za kuendesha vituo vyetu vya habari vya Morning star Radio na Morning Star Television
  3. Taarifa na habari kutotolewa kwa wakati, habari nyingi hutegemewa kutokea kanisani kuja ngazi za juu, habari ikichelewa kufika haiitwi habari tena huitwa taarifa
  4. Ukosefu wa walimu wa kutosha kufundisha masomo ya komputa makanisani.
  5. Makanisa mengi hayana kumbukumbu za kutosha katika kufanikisha ukusanyaji wa Taarifa za ACMS.

MIPANGO YA IDARA KWA MIAKA MITANO MBELE

 

Mipango hii imejengwa kutoka katika maazimio na mapendekezo yaliyopitishwa na kamati ya idara ya mawasiliano ya unioni ya kaskazini mwa Tanzania iliyokaa tarehe 12 – 16 Januari 2015 pamoja na maazimio ya mkutano wa TAiN uliofanyika tarehe 22 – 24 Juni 2015.

 

  1. Mkutano wa TAiN mwaka 2016 utafanyika Dodoma, mkutano huu unategemea kuleta wataalamu na wabunifu wa teknolojia ambao watajadili ubunifu na njia za teknolojia ya mtandao ili kutimiza utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato.
  2. Asilimia 4 ya sadaka ya kuchangia vyombo vya Habari vya Morning Star Radio na Morning Star TV kuendelea kutolewa kwa washiriki wote wa Tanzania
  3. ACMS (Adventist Church Management System) kuanza kutumika katika makanisa mahalia
  4. Kuanzishwa kwa magazeti ya konferensi na Unioni.
  5. Makanisa na Taasisi kuwa na tovuti na ziwe katika mfumo wa netAdventist
  6. Kuwa na vituo vya habari (Media Centers) na Studio katika Taasisi za Kanisa ili kusaidia utayarishaji wa vipindi na pia kuwa na waandishi wa habari katika taasisi hizo.
  7. Kwa kuwa idara hii hutegemea anga moja la Tanzania, ushirikiano baina ya Unioni mbili za Tanzania wapaswa kukuzwa na kuboreshwa kila siku.
  8. Kuwa na mikutano ya wanateknolojia ya habari na mawasiliano kwa ngazi ya Konferensi na Unioni Kila Mwaka.
  9. Kushirikiana na Chuo Kikuu cha Arusha kuanzisha masomo ya Mawasiliano na Umma (Mass Communication)
  10. Kupanua usikivu wa radio na television katika maeneo ya ndani ya nchi ya Tanzania na Afrika mashariki ili kuongeza idadi ya wasikilizaji wa Radio na Television.

 

MWISHO

Idara ya Mawasiliano inatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Unioni ya kaskazini mwa Tanzania kwa kushirikiana pamoja kusimamia kazi na kuboresha kazi katika eneo la kaskazini mwa Tanzania. Tuna imani na viongozi wapya wataendeleza pale tulipoishia na kuboresha pale tulipoanzisha.  Mungu awabariki sana

Na Gideon Msambwa, Mkurugenzi

Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Unioni konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania

2014 – 2015.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference