Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

Kikao cha Maofisa wa Kanisa la Waadventista wa Sabato
katika jimbo kuu la kaskazini mwa Tanzania(NTUC)
kimeanza rasmi Leo February 24/2016.
Akihutubia wajumbe,wafanyakazi na viongozi mbalimbali
kutoka katika majimbo Manne yanayounda Jimbo kuu hilo
Mgeni Rasmi wa kikao hicho Bill Knott ambaye ni mhariri wa
Gazeti la Review & Herald linalomilikiwa na Kanisa hilo ulimwenguni
aliwaasa kutoogopa changamoto zinazojitokeza katika kazi na Maisha
kwa kuwa Mungu ameandaa Jeshi kubwa la Malaika kwa ajili yao.
Katika kikao hicho maalumu Mwenyekiti Wa jimbo hilo la kaskazini mwa Tanzania (NTUC)
Mch na Dr Godwin Lekundayo aliwatambulisha maofisa wawili kutoka
Division ya Afrika mashariki na Kati(ECD),Maofisa wa NTUC
pia maofisa kutoka katika majimbo manne( 4)yanayounda jimbo hilo
kuu ambayo jimbo la Nyanza kusini(SNC),Kaskazini mashariki mwa
Tanzania(NETC) Mara (MC) pamoja Jimbo la Magharibi mwa Tanzania (WTC).
Aidha kikao hicho kina Malengo ya kushauriana na kuelekezana jinsi Maofisa hao
na Wasaidizi wao katika ofisi zao watakavyofanya kazi kwa ufanisi katika muhula
mpya wa kazi.Kikao hicho ambacho kinafanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Ofisi za jimbo kuu hilo (NTUC) kinatarajiwa kuhitimishwa mwishoni mwa Juma hili.© 2018 Northern Tanzania Union Conference