Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

Big- Day Moshi

Posted on Dec 05 2016

Na; Naetwe Kimweri.

Idara ya Wanawake katika jimbo kuu la Kaskazini mwa Tanzania inaendeleza huudua yao ya kufanya machangzo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Raibu ya madawa ya kulevya pamoja waathiria wa ukahaba kinachotarajiwa kuanza kujengwa mapema mwaka 2017.

Machangizo hayo ambayo yamepewa jina la “Big-Day” ya wanawake,mapema jumamosi ya tarehe 03/12/2016 yalifanyika rasmi katika mkoa wa Kilimanjaro,wilayani Moshi katika mtaa wa Pasua na Majengo katika kanisa la Waadventista wa Sabato Majengo, Ambapo waumini kutoka katika makanisa Zaidi ya kumi walifurika katika kanisa hilo ili kuchangia kwa pamoja mradi huu wa Singida.

Katika hotuba yake ya Ibada kuu Mchungaji Godson Willium alisisitiza katika umuhimu wa kusaidia wahitaji katika shida zao mbalimbali nakuzitatua pale inapobidi kwani kwakufanya hivyo tunamtangaza Yesu Kristo kwa vitendo na ndio dini safi inayoelezwa katika Biblia.

Katika kusisitizia suala hili la ujenzi wa kituo hiko cha Raibu ya madawa ya kulevya  na waathirika wa ukahaba,Mhazini mkuu wa Jimbo kuu la Kaskazini mwaTanzania Bwana Dickson Matiko alijaribu kuwasihi wazazi kuwaombea watoto  wao sana kwani ulimwengu unabadilika na hivyo ka kuwatakua katka mikono salama na hivyo kuepuka matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika jamii zetu.

Katika changizo hilo kiasi cha Tsh 6,832,300  Taslimu na  ahadi Tsh.8,850,500/=na pikipiki moja itakayo wasilishwa kabla ya tarehe 31 Desemba.

Changizo hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Union na Division ya Afrika Mashariki na kati akiwemo mama Winfrida Mitekaro kutoka ECD, hawa walishiriki vyema katika kuchangia mradi huo.Big- Day nyingine mjini Moshi inaatarajiwa kufanyika Mei 2017 katika viwanja vya Mashujaa mkoani Kilimanjaro.

0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference