Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

Ministerial convention

Posted on May 03 2017

MKUTANO WA WACHUNGAJI

Mkutano wa wachungaji jimbo kuu Kaskazini mwa Tanzania  umemalizika katika viwanja vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mjini kati Arusha  Tanzania.

Mkutano huo ulidumu kwa siku mbili mfululizo ukiwa na lengo la kuelimisha juu ya  utunzaji na urejeshwaji wa washiriki ndani ya kanisa na mikutano ya Ushirikishwaji kikamilifu kwa kila mshiriki yan Total member Involvent inayo tarajiwa kufanyika mwezi wa sita  nchini Tanzania.

Mkutano huo ulifanyika chini ya Katibu mkuu Dr.Gt NG kutoka mako makuu ya Kanisa General Confrence pamoja na Dr.Allain Corallie kutoka  Jimbo la Afrika Mashariki na Kati (ECD) akiambatana na Mch.Mussa Mitekaro ambaye ni Mkurugenzi wa huduma katika jimbo la Afrika Mashariki na Kati.

 Viongozi hao pia walipata wasaa wa kufika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha nakuonana na Mh.Mrisho Gambo ,na kupata wasaa wakuzungumza nae ikiwa ni ishara ya kudumisha uhusiano kati ya serikali na kanisa.Katika kusisitiza hilo Ofisi za Union ziliwasilisha Tsh.1,500,000/= kama mchango wa kanisa kuendeleza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Monduli mkoani humo.

Mkutano ulimalizilika na viongozi hao walipata nafasi ya kutembelea hifadhi za Taifa za Ngorongoro na vivutio mbalimbali.

 

0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference