Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

GAiN

Posted on May 03 2017

GAiN

Mikutano ya Mawasiliano iliyokua ikifahamika kwa jina la TAiN, yaani Tanzania Adventist Internet network sasa inakujia kwa jina la GAiN-TZ yaani Global Adventist Internet Network-Tanzania. Likiwa ni jina lenye kujumuisha  mikutano ya mawasiliano  kwa ulimwengu mzima kwa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

Mwaka huu mkutano wa GAiN utafanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa JB-Belmont, mount fair kuanzia tarehe 15 mpaka tarehe 20 mwezi wa tano mwaka 2017.

Mkutano huu wa kimataifa utakuwa na wakufunzi kutoka katika ngazi za kanisa za juu pamoja na wataalamu waliobobea katika fani ya mawasiliano kiulimwengu, Viongozi wamawasiliano kutoka makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato yaani General Confrence wakiambatana na viongozi kutoka jimbo la Afrika Mashariki na Kati yaani (ECD)Pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nchini mwetu.

 Pia kutakua na uzinduzi wa filamu mbili za kanisa la waadventista Wasabato zitakazo zinduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika katika nchi yetu ya Tanzania , ambazo zinafahamika kwajina la “Creation’ pamoja na “The opposite.”.

Wahusika katika mkutano huu ni pamoja na maofisa wote wa kanisa,wachungaji wote,wazee wa makanisa wote,makarani wote wa kanisa,wakuu wa mawasiliano kanisani,wataalamu wa IT,waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa mawasiliano.

Kiingilio katika mkutano huu ni Tsh 50,000/= tu na gharama zingine zitakua juu ya mtu mwenyewe. Mwisho wa kutoa kiingilio ni tarehe 10/05/2017,
Usipange kukosa karibu tujumuike pamoja kumaliza kazi ya Bwana kwa njia ya mawasiliano
/>

0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference