Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

GAiNTZ2017

Posted on May 24 2017

 Akihutubia Zaidi ya wajumbe 500 waliohudhuria Mkutano Wa Wanataaluma waadventista Wa Sabato Tanzania (GAiN TANZANIA ) jijini Mwanza Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo kuu Kaskazini mwa Tanzania Mch ,Dr Godwin Lekundayo amesema kuwa kila mmoja anaefahamu jukumu la mkristo la kueneza injili anapaswa kutumia  mitandao ya jamii kuwafikia watu walioko Mbali  ili wamjue Yesu.
        Dr Lekundayo ameeleza kuwa  wachungaji wanaoamini na kufikiri kuwa kutumia Facebook,Instagrum Twitter na mitandao mingine katika kuchunga waumini na katika kueneza Injili ni dhambi wanapaswa kutubu.Ameeleza kuwa Kwa kizazi na jamii ya sasa hakuna njia nyingine rahisi ya kutumia katika injili kwa sababu idadi kubwa ya watu kwa sasa wanatumia muda Mrefu katika mtandao hivyo ili kuwafikia ni lazima kutumia Mitandao ya jamii.
        Mkutano huu umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali Wa kanisa la waadventista wa  sabato kutoka katika majimbo makuu ya kanisa hilo Nchini Tanzania.
         Mkutano huo unaohusisha wanataaluma Wa Tehama,watunza kumbukumbu za kanisa katika ofisi za Majimbo makuu na madogo,taasisi ,wachungaji na makarani Wa makanisa Mahalia umeanza hii Leo May 15 ,2017 jijini mwanza na utahitimishwa may 20 ,2017.
         Aidha mkutano huu una wazo Kuu la kuandaliwa kwa ajili ya Utume ukilenga wito mkuu  Wa Manisa ulimwenguni Wa kila mmoja kushiriki kikamilifu katika Injili (TMI)Total member involvement.0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference