Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu
Tarehe 21 Machi 2015 ni siku maalumu ya vijana wote wa kanisa la Waadventista wa Sabato duniani, siku hiyo vijana wote wakiadventista watatoka kanisani kwenda kutoa huduma kwa wahitaji pamoja na kuonesha matendo ya huruma kwa watu mbalimbali wenye mahitaji.
Union ya kaskazini mwa Tanzania imechagua jiji la Arusha kuwa kituo kikuu cha kuonesha matendo ya huruma kwa wahitaji.
Ratiba ya siku ya Sabato ya tarehe 21 ni Kama Ifuatavyo

3:30 Asubuhi
Kukutana kanisani au sehemu iliyopangwa
Kuwa na ibada fupi
Ombi
Matangazo

4:00 Asubuhi
Kwenda kutenda matendo Mema

6:30 Mchana
Chakula cha mchana

8:00 mchana
Kuendelea na Matendo MemaContinue with Act of Kindness
Kujihusisha na Mipango

11:00 Jioni
Kukutana kwa taarifa
Chakula cha jioni
Kutoa sifa
Kutuma picha na Taarifa kwa vyombo vya habari 


Mch. Elias Kasika (kulia) mkurugenzi wa idara ya vijana Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania, akiwa na Mch. Azza Nyamakababi ( Kushoto) Mkurugenzi wa idara ya uwakili na chaplensia konferensi ya kaskazini mashariki mwa Tanzania na Ndugu Bonphas Mshana Mwenyekiti Msaidizi wa vijana katika jiji la Arusha, wakipanga ratiba ya siku ya vijana duniani itakayofanyika tarehe 21 Machi 2015. Tuwaombee Mungu azidi kuwatumia tunapojiandaa kuwahudumia wahitaji kwa kuwatendea matendo ya huruma katika siku hii muhimu.
© 2018 Northern Tanzania Union Conference