Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

Kanisa la Waadventsta Wasabato la shiriki katika kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi huko Kagera.

Posted on Oct 23 2016

Kanisa la Waadventista Wasabato kupitia shirika la maendeleo na misaada ADRA  Tanzania,limetoa msaada wa Thamani ya shilingi milioni arobaini na sita kwa mkoa wa Kagera,kutokana  na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani huko.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kwa niaba ya Kanisa, kaimu mkurugenzi wa ADRA Tanzania ndugu Elamu Bunde, amesema Kanisa limeguswa na tatizo walilolipata wananchi wa Kagera na kuongeza kuwa Kanisa litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ili kuhakikisha maisha ya wahanga wa tetemeko yanarudi katika hali ya kawaida.

Msaada uliotolewa na Kanisa la Waadventista wa Sabato kupitia shirika la ADRA umehusisha shilingi milioni kumi na sita iliyotolewa kupitia akaunti maalumu ya maafa ya mkoa na shilingi milioni thelathini iliyo nunulia vifaa kama blanketi na vyandarua.

Akipokea msaada huo mkuu wa Mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu Salumu Mustafa Kijuu, amelishukuru kanisa la Waadventista  wa Sabato  kwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa msaada mkubwa na kuongea kuwa hiyo ndiyo dini ya kweli.Kijuu  ameongoza kuwa Mkoa wa Kagera bado unahitaji msaada mkubwa kutokana na athari kubwa zilizojitokeza katika miundo mbinu ya huduma za kijamii kama barabara, shule na hosptali.

Aidha mkuu wa Mkoa amezitaja baadhi ya athari hizo kuwa ni pamoja na vifo vya watu 17, majeruhi 440 kati ya hao 23 wamefanyiwa upasuaji mbalimbali kutokana na kuvunjika baadhi baadhi ya viungo vya miili yao na mpaka sasa majeruhi sita bado wako hospitalini , Katka tetemeko hilo jumla ya majengo 2072 yalianguka kabisa, 16595 yamepata  mipasuko hatarishi na hayafai kukaliwa na watu, na jumla ya nyumba 9927 zimepata mipasuko inayofaa kurekebishwa.

Hata hivyo Kijuu hakutaka kufafanua juu ya Kiasi gani cha fedha kiliingizwa kwenye akaunti bandia  ya maafa iliyofunguliwa kinyme na utaratibu wa serikali na baadhi ya watumishi wa mkoa kwa madai kuwa  jambo hilo lipo mahakamani.  Kijuu aliongeza kuwa wananchi walioathirika wanapaswa kuanza kukarabati nyumba zao kwani Serikali bnayo itaanza kukarabati miundombinu ya huduma za kijamii.

Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa tathimini inaonyesha mkoa bado unahitaji kiasi cha shilingi milioni kumi ili kurejesha miundo mbinu ili haribika.

Mkoa wa Kagera ulipata tetemeko l ardhi lenye ukuwa wa 5.9 kipimo cha Ritcher lililopiga chini umbali wa km 40 septemba 10 na kupelekea vifo vya watu 17, na athari nyingine mbalimbali zilizopelekea  Serikali kutangaza Mkoa huu kuwa Mkoa wa maafa unaohitaji msaada wa dhararura.


© 2018 Northern Tanzania Union Conference