Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

BIG-DAY kwaajili ya vyombo vya habari vya kanisa la waadventista Wa Sabato ya fanyika huko Tanga.

Posted on Nov 01 2016

Waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato jijini Tanga wajitokeza kwa wingi katika kuchangia vyombo vya habari vya kanisa lao vya Morningstar Redio pamoja na televisheni, ili kuviimarisha na kuongezaa usikivu wake katika maeneo tofauti nchini na hata nje ya nchi.

Changizo hilo lililofanyika katika kanisa la Waadventista Wasabato  Kana na kualika Zaidi ya makanisa kumi na tano yatokayo katika mitaa minne ya jiji hilo la Tanga ambayo ni Mtaa wa Kana, Kange,Makorora pamoja na Mtaa wa Mabawa. Ambayo kwa ujumla wake walichangia kiasi cha Tsh. 13,380,850/= milioni kumi na tatu laki tatu na themanini elfu na mia nane hamsini.

Aidha katika kushukuru waumini hao wa jiji laTanga Mkurugenzi wa vyombo vya habari Mch.Christopher Ungani alisema katika machangizo yote yaliyowahi kufanyika jiji la Tanga limefanya kwa kiasi kikubwa kulingana na muda waliopewa taarifa, na hiyo inaonyesha jinsi wanavyo jitoa kwa ajili ya kufanya kazi ya Mungu.

Changizo hilo ambalo hufanyika mara kwa mara katika maeneo tofauti tofauti nchini Tanzania lilihudhuriwa na Katibu wa jimbo dogo la Kaskazini mashariki mwa Tanzania Mch.Musa Nzumbi ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa jimbo kuu la Kakazini mwa Tanzania Dkt. Godwin Lekundayo.

Hata hivyo waumini wa kanisa la Waadventisa Wasabato jijini humo walishukuru kwa viongozi hao wa mawasiliano wa majimbo yote mawili kufika mkoani humo kwani ni chachu ya wao kuendeleza kutoa kwaajili ya vyombo vyao vya habari kwani wanatamani Redio hiyo ya Morning star kusikika huko kwani ni kwa muda sasa haipatikani humo.


0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference