Seventh-Day Adventist Church

Northern Tanzania Union Conference

Menu

Mahafali ya Chuo Kikuu cha Arusha

Posted on Nov 25 2016

Na; Naetwe Kimweri

Chuo kikuu cha Arusha kilichopo chini ya kanisa la waadventista Wasabato kimefanya mahafali ya 10( kumi) tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 2003, Mahafali hayo yalikuwa yamejumuisha wahitimu wa ngazi mbali mbali ikiwemo wa shahada ya kwanza kwa  vitivo tofauti tofauti na shahda ya uzamili( masters) pia kwa vitivo mbali mbali.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi wa kuu wa kanisa hilo kutoka katika Union zote Mbili ya kaskazini  na ya kusini.

Katika kuadhimisha mahafali hayo Mkuu wa chuo hiko Dr. Godwin Lekundayo ambaye pia ni mwenyekiti wa kanisa jimbo kuu kaskazini mwa Tanzania aliwaasa wanafunzi katika kufanya kazi kwa bidii lakini pia katika kumtegemea Mwenyezi Mungu aliyewafikisha katika hatua hiyo kubwa katika maisha yao.Aidha Mkuu wa chuo hiko aliwatunuku zaidi ya wanafunzi 1000 waliofuzu mafunzo ya kwa ngazi mbalimbali ikiwemo Cheti, Stashahada, shahada na shahada ya pili (masters).

0 comments

Add Comment
 

Add your comment

To add a comment you need to login or register.

© 2018 Northern Tanzania Union Conference